MICHEZO:WALLACE KARIA RAISI MPYA TFF
MICHEZO:WALLACE KARIA RAISI MPYA TFF
Timu nzima ya STAR SMART TV ONLINE ilipiga kambi kuhakikisha inapata matokeo ya uchaguzi wa Shirikisho la soka Tanzania. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu imefanikiwa kukuletea matokeo yote,
Rais mpya wa TFF ni Wallace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya na wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.
Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.
Nafasi
ya Makamu wa Rais, Wambura alipata kura 85, alishindana na Mulamu
Ngh'ambi aliyepata kura 25, Mtemi Ramadhan kura 14, Richard Selasela
kura mbili.
Wajumbe wa kamati ya utendaji walioshinda
kutoka katika Kanda 13 ni pamoja na Kanda 13(Dar es Salaam) mshindi ni
Lameck Nyambaya aliyepata kura 41. Kanda 12 (Kilimanjaro&Tanga)
mshindi ni Khalid Abdallah aliyepata kura 70.
Kanda ya
11(Pwani&Morogoro) mshindi ni Francis Ndulane aliyepata kura 70,
Kanda ya 10 (Dodoma&singida) mshindi ni Mohammed Aden aliyepata kura
35, Kanda ya 9 (Lindi&Mtwara) mshindi ni Dastan Mkundi amepata kura
74.
Kanda ya 8 (Njombe&ruvuma) mshindi ni James
Mhagama aliyepata kura 60, Kanda ya 7 (Mbeya & Iringa) mshindi ni
Elias Mwanjala aliyepata kura 61, Kanda ya 6 (Katavi&Rukwa) mshindi
ni Kenneth Pesambili aliyepata kura 72
Kanda ya 5
(Kigoma&Tabora) mshindi ni Issah Bukuku aliyepata kura 80, Kanda ya
4 (Arusha&Manyara) Sarah Chao aliyepata kura 57, Kanda ya 3
(simiyu&shinyanga) mshindi Mbasha Matutu aliyepata 67, Kanda ya 2
(Mwanza&Mara) Vedastus Lufano alipata kura 67, Kanda ya 1
(Kagera&Geita) mshindi alikuwa Salum Chama alipata kura
90.
Ahadi 11 za Karia
Karia alizindua kampeni na kutaja vipaumbele vyake 11 atakavyohakikisha anavisimamia kikamilifu.
Vipaumbele
hivyo vilivyotajwa ni nidhamu ya muundo na mfumo, maendeleo ya vijana,
wanawake na soka la ufukweni, mafunzo na ujenzi wa uwezo, mapato,
uwezeshaji na nidhamu ya fedha, miundombinu na vifaa na maboresho ya
bodi ya ligi.
Vingine ni ushirikiano wa wadau, udhamini
na masoko, maboresho ya mashindano, uimarishaji mifumo ya kumbukumbu na
ufanisi wa waamuzi.
Karia alisema kuwa atahakikisha vipaumbele hivyo vinafanyiwa kazi muda mfupi baada ya yeye kuingia madarakani.
0 comments :