Picha,Floyd Mayeweather ameshinda pambano dhidi ya Conor Mcgregor kwa TKO katika raundi ya 10

Picha,Floyd Mayeweather ameshinda pambano dhidi ya Conor Mcgregor kwa TKO katika raundi ya 10


Bondia Floyd Mayeweather ameshinda pambano dhidi ya Conor Mcgregor kwa TKO katika raundi ya 10.
Pambano hili lilikuwa miongoni mwa mapambano makubwa ya ngumi kufanyika duniani sababu ya ukubwa wa wapiganaji hawa, Conor akiwa ni champion wa MMA na Floyd akiwa ni rekodi ya kutopigwa katka mapambano 50 kwenye maisha yake ngumi
Mpaka Round ya 5 McGregor alionekana kuwa kwenye hali nzuri ila baada ya hapo alionekana kuchoka na kukata tamaa kabisa ba kukubali ngumi kutua usoni kwake kila mara.
Baada ya refa kusimamisha pambano Conor alilalamika kuwa bado alikuwa na nguvu ya kuendelea, kwenye mahojiano mwisho wa pambano alisema “Nimepigwa sababu ya uchovu, nilichoshwa sana na mazoezi, ila refa alitakiwa kuacha pambano liendele”.

STARSMART TV: REHMA NURSERY & PRIMARY SCHOOL.

STARSMART TV: REHMA NURSERY & PRIMARY SCHOOL.

ALICHOANDIKA DIVAH WA CLOUDS FM KUHUSU SEDUCE ME YA ALI KIBA

ALICHOANDIKA DIVAH WA CLOUDS FM KUHUSU SEDUCE ME YA ALI KIBA

Mtangazaji maarufu wa Radio Diva Loveness Love [Clouds Fm] ametmia twitter kuandika ujumbe mfupi kuhusu rekodi mpya ya Ali Kiba #SeduceMe iliyotayarishwa na Producer Man Water.
Diva anasema >>Seduce me ya Alikiba ni Kama Pedi za Kike lazima Uvae , Mziki umeenda shule Huu #seduceme like what da hell
POVU LA NAY WA MITEGO KWA MOND, ALI KIBA NA OMMY DIMPOZ

POVU LA NAY WA MITEGO KWA MOND, ALI KIBA NA OMMY DIMPOZ

Mambo yamemfika HAPAA Nay wa Mitego na kuamua kutoa POVU kali kuhusu Beef la Ommy Dimpoz, Ali Kiba Vs Diamond Platnumz.
Ikiwa ni stori kubwa kwenye bongo fleva Tanzania, Sio jambo jipya kwa mfuatiliaji wa muziki kusikia beef hili la Ali Kiba ba Diamond, ambalo leo limepelekea Ommy Dimpoz kuweka picha ya Mama yake Diamond kwenye IG na kuandika maneno makali.
Well Post hio imepondwa na wengi sababu beef hili haliwahusu wazazi wa wasanii hawa..Rapa Nay wa Mitego ambaye ni rafiki wa wasanii wote hawa kaandika ujumbe huu….”Gombaneni, Loganeni Mpaka Muuwane… Napenda Kusikia Challenge Kwenye Game, Ila Tusiwaingize Wazazi Wetu🙏🏿 Please. Tutukananeni Matusi Yote Wenyewe Kwa Wenyewe Ikibidi Piganeni Kabisaaaa Atakae Kufa Tutazika na Itakua Historia Kama Big na Pac. Ila Kuwaingiza Wazazi ni U #Maku 
Sipo Upande Wowote,Si #Kiba #MondWala #Ommy. Endeleeni na Vita yenu Kama Wanawake Mmechukuliana Mabwana. Ila Swala la Wazazi Mnavuka Mipaka #Makunyie.!
RAPPER AOMBWA ATENGENEZE WMBO WA TAIF WA MAREKANI

RAPPER AOMBWA ATENGENEZE WMBO WA TAIF WA MAREKANI

Baada ya mashabiki kumuomba rapa wa kundi la Migos Quavo kutengeneza wimbo wa mpya wa taifa la Marekani ,staa huyu amejibu na kutoa vigezo vyake.
Quavo amesema “Ningependa kutengeneza wimbo pya wa taifa ila nitapenda zaidi kama nitatengeneza wimbo wa taifa wa mwaka 2017 kwaajili ya kila mtu na usio na ubaguzi, kitu kinachowakilisha kila mtu”
Quavo anasema kwanza lazima akusanye wasanii waimbaji wazuri sana na apewe muda mzuri wa kuandika wimbo huu.
Wimbo wa taifa wa Marekani unaitwa ‘The Star-Spangled Banner’ una miaka 203 na uliandikwa na mshairi Francis Scott Key.
DADA WA DIAMOND AINGILIA KATI BIFU LA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ

DADA WA DIAMOND AINGILIA KATI BIFU LA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ

Baada ya Ommy Dimpoz Kumtolea Povu Diamond Platnumz kwa kupost picha akiwa na Mama yake na Kujiita Baba yake Diamond, Dada wa Diamond amekerwa na jambo hili na kuamua Kuingilia Kati bifu hilo.
Esma Platnumz ameandika ujumbe huu kwenye picha aliyoweka Ommy Dimpoz….
MWANA FA: BIFU LA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ LINACHANGAMSHA

MWANA FA: BIFU LA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ LINACHANGAMSHA

Msanii wa muziki wa hip hop, Khamisi Mwinjuma, maarufu mwana FA amedai bifu kati ya Diamond na Ommy Dimpoz ni vitu ambavyo vinahitaji kwenye muziki kwa kuwa vinachangamsha game.
diamond



















Diamond na Ommy Dimpoz hivi karibuni waliingia kwenye bifu zito hali ambayo ilipelekea wawili hao kumtupiana maneno ya kashfa katika mitandao ya kijamii.
Akiongea na gazeti la Habari Leo wiki hii, Mwana FA alisema bifu la wasanii hao linachangamsha tasnia ya muziki na kusisitiza muhimu ni kudhibiti wasizuriane.
“Unajua hakuna kitu kisichokuwa na ushindani, mfano wewe upo STAR SMART lazima mtakuwa na washindani wenu, mnachotakiwa kufanya ninyi waandishi ni kujizuia msizuriane,” alisema FA.
“Inachangamsha muziki unapata wa kuwazungumzia, kukiwa na ushindani wa hapa na pale sifikiri kama ni kitu unachoweza kukizuia, game ikiwa rafiki sana nayo inakuwa haiwezi kuburudisha, haiwezekani mashabiki wawe wote wa wanamuziki wote hakuna kitu kama hicho,” aliongeza.
Pia rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Dume Suruali’ amedai kwa sasa bado ana mambo mengi ya kufanya katika kuendeleza muziki wake lakini pia kuendeleza familia yake pamoja na masuala ya biashara.
MALAIKA LOUNGE: MATUKIO YANGA FT SIMBA

MALAIKA LOUNGE: MATUKIO YANGA FT SIMBA



Gila The Boss akitambulisha Nyimbo yake mpya aliyofanya na Chid Benz

Gila The Boss akitambulisha Nyimbo yake mpya aliyofanya na Chid Benz

MANSU LI: NASUBIRI TU MWEZI WA KUMI NINA SUPRISE KWA WATU WA DODOMA

MANSU LI: NASUBIRI TU MWEZI WA KUMI NINA SUPRISE KWA WATU WA DODOMA

OG MUSIC SOUND: Njoo upate ushauri juu ya gari lako

OG MUSIC SOUND: Njoo upate ushauri juu ya gari lako

MICHEZO:WALLACE KARIA RAISI MPYA TFF

MICHEZO:WALLACE KARIA RAISI MPYA TFF

Timu nzima ya STAR SMART TV ONLINE ilipiga kambi kuhakikisha inapata matokeo ya uchaguzi wa Shirikisho la soka Tanzania.  Baada ya kusubiri kwa muda mrefu imefanikiwa kukuletea matokeo yote,
Rais mpya wa TFF ni Wallace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya na wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.




Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.

Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.
Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.
Nafasi ya Makamu wa Rais, Wambura alipata kura 85, alishindana na Mulamu Ngh'ambi aliyepata kura 25, Mtemi Ramadhan kura 14, Richard Selasela kura mbili.
Wajumbe wa kamati ya utendaji walioshinda kutoka katika Kanda 13 ni pamoja na  Kanda 13(Dar es Salaam) mshindi ni Lameck Nyambaya aliyepata kura 41. Kanda 12 (Kilimanjaro&Tanga) mshindi ni Khalid Abdallah aliyepata kura 70.
Kanda ya 11(Pwani&Morogoro) mshindi ni Francis Ndulane aliyepata kura 70, Kanda ya 10 (Dodoma&singida) mshindi ni Mohammed Aden aliyepata kura 35, Kanda ya 9 (Lindi&Mtwara) mshindi ni Dastan Mkundi amepata kura 74.
Kanda ya 8 (Njombe&ruvuma) mshindi ni James Mhagama aliyepata kura 60, Kanda ya 7 (Mbeya & Iringa) mshindi ni Elias Mwanjala aliyepata kura 61, Kanda ya 6 (Katavi&Rukwa) mshindi ni Kenneth Pesambili aliyepata kura 72
Kanda ya 5 (Kigoma&Tabora) mshindi ni Issah Bukuku aliyepata kura 80, Kanda ya 4  (Arusha&Manyara) Sarah Chao aliyepata kura 57, Kanda ya 3 (simiyu&shinyanga) mshindi Mbasha Matutu aliyepata 67, Kanda ya 2 (Mwanza&Mara) Vedastus Lufano alipata kura 67, Kanda ya 1 (Kagera&Geita) mshindi alikuwa Salum Chama alipata kura 90.                      
Ahadi 11 za Karia
Karia alizindua kampeni  na kutaja vipaumbele vyake 11 atakavyohakikisha anavisimamia kikamilifu.
Vipaumbele hivyo vilivyotajwa ni nidhamu ya muundo na mfumo, maendeleo ya vijana, wanawake na soka la ufukweni, mafunzo na ujenzi wa uwezo, mapato, uwezeshaji na nidhamu ya fedha, miundombinu na vifaa na maboresho ya bodi ya ligi.
Vingine ni ushirikiano wa wadau, udhamini na masoko, maboresho ya mashindano, uimarishaji mifumo ya kumbukumbu na ufanisi wa waamuzi.
Karia alisema kuwa atahakikisha vipaumbele hivyo vinafanyiwa kazi muda mfupi baada ya yeye kuingia madarakani.
A FM: TUMEJIPANGA KUMSAPOTI MR FRANK TAREHE 01/09/2017 IWE SIKU YA KIPEK...

A FM: TUMEJIPANGA KUMSAPOTI MR FRANK TAREHE 01/09/2017 IWE SIKU YA KIPEK...

PICHA:BAADHI YA WAGOMBEA WA UCHAGUZI MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA

PICHA:BAADHI YA WAGOMBEA WA UCHAGUZI MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA





UCHAGUZI: ALI MAYAY TEMBELE NITAIBUA DIRA YA MAENDELEO

UCHAGUZI: ALI MAYAY TEMBELE NITAIBUA DIRA YA MAENDELEO

NANE NANE: REHMA PRE & PRIMARY SCHOOL TUNALEA KUANZIA MTOTO MWAKA 1

NANE NANE: REHMA PRE & PRIMARY SCHOOL TUNALEA KUANZIA MTOTO MWAKA 1

NANENANE :TIGO:TUMEJIPANGA KUWAHUDUMIA

NANENANE :TIGO:TUMEJIPANGA KUWAHUDUMIA

NANENANE :TIGO:TUMEJIPANGA KUWAHUDUMIA

NANENANE :TIGO:TUMEJIPANGA KUWAHUDUMIA

STARSMART TV: UZINDUZI WA GYM MPYA YA SHABBY(KTN FITNESS)

STARSMART TV: UZINDUZI WA GYM MPYA YA SHABBY(KTN FITNESS)

 
Copyright © 2015. STAR SMART BLOG TZ
Blogger Templates